JOHN SIMKOKO ASEMA MTIBWA NA YANGA WATACHEZA JAMHURI
Meneja wa uwanja wa Jamhuri ulioko mkoani Morogoro,John Simkoko amesema kwamba kwa sasa wanaendelea na ukarabati wa uwanja huo ili uweze kutumika katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga unaotaraji kupigwa siku ya tarehe tano ya mwezi wa tatu mwaka huu.
Simkoko amesema kwamba anaamini ukarabati huo hautachukua muda mrefu,kwani ni marekebisho macheche ndio yanayoendelea kufanyiwa kazi kwenye uwanja huo.
Aidha ameweka bayana juu ya maamuzi ya TFF kuusimamisha uwanja huo,ambapo amedai kuwa uwanja huo umesimamishwa kwa mechi za ligi kuu pekee lakini mechi nyingine zinaendelea kuchezwa uwanjani hapo ikiwemo michezo ya ligi daraja la kwanza.
Post a Comment