OTIENO AJINASIBU KUIFUNGA MTIBWA KESHO

Kocha wa timu ya Afrika Lyon Charse Otieno amesema kwamba kikosi chake kimejiaandaa vyema kuwakabili Mtibwa Sugar hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Otieno amesema kwamba leo hii wachezaji wake wamekamilisha mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo na jambo la faraja kwake ni kuona kila mmoja ana hamasa ya kutosha kuelekea kwenye pambano hilo linalotaraji kuwa na ushindani mkubwa kutokana na nafasi waliyo nayo kwenye msimamo wa ligi.

No comments