MASHABIKI WA YANGA WAONYESHA MAHABA KWA MANJI

Baadhi ya mashabiki wa timu ya Yanga leo hii kwa mahaba mazito ya mwenyekiti wa klabu yao,Yusuph Manji waliweza kujitokeza katika kituo kikuu cha Polisi jijini Dar es salaam ili kutaka kufahamu kinachoendelea juu ya mwenyekiti wao aliyewasili leo hii kituoni hapo kunakoa mishale ya saa tano asubuhi.

Manji ametimiza ahadi yake aliyoitoa hapo jana mbele ya waandishi wa Habari akijibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda kuwa yeye ni miongoni mwa watu ambao wanatuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.

Akiongea na waandishi wa Habari siku ya jana Manji alisema kwamba yeye angewasili leo hii Polisi kama alivyofanya licha ya wito wake kutakiwa kulipoti hapo kesho.

Mashabiki hao kwa nyakati tofauti walionekana wakilanda laanda pembezoni mwa kituo hicho huku baadhi yao wakidiriki kulifanyia usafi gari la Manji.

Hata hivyo idadi ya watu iliongezeka baada ya kufika kwa mchungaji Gwajima ambae nae anahusishwa na tuhuma hizo za madawa ya kulevya  aliyeongozana na watu saba.


No comments