KUFUZU KWA SERENGETI BOYS MALINZI AMPONGE MAGUFULI

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limepokea kwa furaha kubwa maamuzi yaliyotolewa na kamati ya utenda ya CAF ya kuipa Tanzania nafasi ya kucheza fainali za vijana za Afrika chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika nchini Gaboni kuanzia tarehe 21 ya mwezi wa tano mwaka huu.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Rais wa TFF,Jamali Malinzi amesema shirikisho hilo limeridhishwa na maamuzi hayo kwani dhamira yao ya kucheza fainali hizo zimetimia licha ya kukutana na vikwazo vingi ambavyo vilionekana dhahirisha kusitisha mpango huo.

Malinzi amesema kwamba Shirikisho la mpira wa miguu TFF,linawapongeza wadau wote wa mpira sambamba na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa jitihada kubwa ambazo wamezifanya kuhakisha Serengeti Boys inafanikiwa kufuzu kwa fainali hizo za vijana.

No comments