MKWASA AREJEA YANGA KWA MAJUKUMU MENGINE

Uongozi wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara,timu ya soka ya Yanga leo hii umemtamburisha aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charse Boniphace Mkwasa kuwa katibu mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clementi Sanga amesema kwamba uongozi umeamua kumpa majukumu Mkwasa kutokana na uzoefu wake alio nao katika sekta ya michezo hivyo anaamini mchango wake utakuwa na tija kubwa katika klabu hiyo.


Sanga amesema kwamba awali nafasi hiyo imekuwa ikishikiliwa na Baraka Deusdedit aliyekuwa anakaimu,lakini kwa sasa uongozi umempa majuku ya kuwa mkurugenzi wa fedha ili kuendelea na majukumu hayo kwa lengo la kuboresha mipango ya timu.

"Mtakumbu kuwa kwa muda mrefu Baraka alikuwa ana kaimu nafasi hii wakati tunahangaika michakato mingine ya kumpata alifanya kazi vizuri na kwa ujumla wake mnadhani mafanikio yake yote ambayo tumefanikiwa amefanya vizuri nafasi hiyo tunamshukuru sana lakini pia atarudi kwenye nafasi yake ya zamani ya ukurugenzi wa fedha wa klabu ya Yanga kwa hiyo nitumie nafasi hiyo kuwataarifu mashabiki na wanacha wetu kuwa Charse Boniphace Mkwasa kuanzia sasa ndie katibu wetu mkuu"alisema Mkwasa.

No comments