MKWASA AKILI KUTOACHANA NA UKOCHA

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba bado hajatangaza rasmi kufundisha mpira wa miguu licha ya kuingia katika majukumu mengine ya maswala ya uongozi.

Mkwasa alisema kwamba kwa sasa ataheshimu mkataba wake ndani ya klabu ya Yanga kama katibu mkuu, hivyo kama kuna timu itahitaji huduma zake ataweza kurejea kwenye majukumu ya ufundishaji wa mpira wa miguu lakini hadi hapo uongozi utakaporidhia.

Siku ya jana makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Clement Sanga alimtamburisha Mkwasa mbele ya waandishi wa Habari kuwa ndiye katibu mkuu wa klabu hiyo,hivyo kukaibuka maswali kwa baadhi ya wadau wa mpira wa miguu juu ya hatma yake ya ukocha.

No comments