AZAM KUCHEZA NA MAMELOD SUNDOWNS TAIFA

Wakati klabu za Simba na Yanga zikishindwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa klabu bingwa barani Afrika Mamelod Sundowns,uongozi wa klabu ya Azam ya jijini Dar es salaam umesema kwamba kikosi chao hapo kesho kunako mishale ya saa moja usiku kinataraji kushuka dimbani kucheza na mabingwa hao wa Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Afisa Habari wa Azam FC,Jafary Idd amesema kwamba ingawa awali hawakuwemo kwenye mipango ya kucheza mchezo huo sambamba na kutomfahamu mratibu wa mchezo huo kwa upande wao wameamua kucheza kwa ajili ya kulinda ushirikiano kwa nchi husika pamoja na klabu.

Alisema kwamba wanacheza mchezo huo huku wakibanwa na ratiba ya ligi kuu ya Tanzania bara kwani siku ya jumamosi watacheza mchezo wa ligi lakini kwa kutambua mpango huo wameamua kufanya hivyo kwa ajili ya kudumisha umoja wao.

Jafary alisema kwamba katika mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watawakosa huduma za wachezaji wao wawili muhimu John Boko pamoja na Stephen Kingue ambao hawa wote ni majeruhi.

No comments