ZANZIBAR WAAMINI WATAFANIKIWA CAF


Katibu mkuu wa chama cha soka cha Zanzibar ZFA Mohd Ally Hilaly,amesema kwamba Zanzibar ina matumaini makubwa ya kupata uwanachama kamili wa CAF hapo tarehe 16 ya mwezi march.

Mohd amesema kwamba kutokana na mikakati iliyopo na juhudi zinazoendelea kufanywa na TFF,pamoja na ZFA anaamini jambo hilo litafanikiwa kwa upande wao.

Amesema kwamba endapo watafanikiwa kwa wao kutambulika kuwa wanachama kamili wa CAF basi anaamini Zanzibar itapiga hatua kubwa kwenye sekta ya michezo kwani wana mipango mingi wamepanga kuifanya pindi wapatapo nafasi hiyo.

No comments