HAJIBU NA MKUDE BADO WAPOWAPO SIMBA

Uongozi wa klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam,umeweka bayana juu ya wachezaji wao wawili ambao mikataba yao imeelekea ukingoni,Ibrahim Hajibu pamoja na Jonasi Mkude.


Kaburu ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba swala mchezaji Ibrahimu Hajibu bado ataendelea kusalia katika klabu hiyo kwa kuwa licha mkataba kuelekea ukingoni lakini bado hawajapata ofa yeyote licha ya awali mchezaji huyo kwenda kufanya majalibio nje ya nchi.

Kuhusu swala la Jonasi Mkude,amesema kwamba mchezaji huyo nae ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo lakini wamepata taarifa kuwa ifikapo mwezi wa sita anatarajiwa kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwa mujibu wa meneja wa mchezaji huyo.

No comments