EMMANUEL OKWI AVUNJA MKATABA KWA MARA NYINGINE

Mchezaji wa zamani wa wekundu wa Msimbazi timu ya soka ya Simba,Emmanuel Okwi ameachana rasmi na timu yake ya Sonderjyske Fodbold ya Denmark,baada ya pande hizo zote mbili kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba.

Mkurugenzi wa klabu hiyo Jorgen Haysen,amesema kwamba uamuzi huo umefanyika baada ya Okwi kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi cha timu hiyo.

No comments