MCHEZAJI AFRIKA SPORT AJIUNGA NA ZANACO

Klabu ya Zanaco ya Zambia leo hii imefanikiwa kukamilisha uhamisho wa mchezaji Ayubu Ruben Rianga kwa mkopo wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Wakala wa wachezaji anaetambulika na FIFA,Jamali Kisongo ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba Rubeni aliyekuwa anaitumikia klabu ya Afrika Sport ya Tanga amepata nafasi hiyo ya kucheza soka kwenye klabu hiyo baada yaye kuwa karibu na viongozi mbalimbali ambao wanafahamika katika soka.

Kisongo amesema kwamba kukamilika kwa uhamisho huo,kutakuwa na tija kubwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu,kwani huenda baadae akawa chachu ya kuwa msada kwenye timu ya Taifa.

Amesema kwamba nchi nyingi ambazo zina maendeleo kwenye timu zao za taifa ni pamoja na kuwa na wachezaji wengi ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi,hivyo kwa Tanzania kuongezeka kwa wachezaji ni faida kubwa.

No comments