HANS AKUBALI KUWA MKURUGENZI WA UFUNDI WA YANGA

Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans van der Pluijm amekubali kuwa mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo baada nafasi yake kuchukuliwa na kocha Mzambia George Lwandamina.

Hans amesema kwamba yeye ameridhia nafasi hiyo ya kuwa mkurugenzi wa ufundi kwa sababu yeye ni muumini mzuri wa mchezo wa mpira wa miguu na amekubaliana na mazungumzo yaliyohusisha pande mbili kati yake pamoja na uongozi wa klabu ya Yanga.

Mapema leo hii uongozi wa Yanga umetoa taarifa ya kuingia makubaliano na kocha Mzambia George Lwandamina kuwa kocha mkuu wa timu hiyo akirithi majukumu ya Hans van der Pluijm kwa kile kinachodaiwa kuwa na wigo mpana katika benchi la ufundi kwa maendeleo ya timu.

No comments