MTIBWA SUGAR WAANZA RASMI MAANDALIZI YA MZUNGUKO WA PILI

Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro tayari kimeshaanza kambi kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Afsa Habari wa Mtibwa Sugar Tobiasi Kifaru amesema kwamba nia yao ni kuona kikosi cha timu hiyo kinafanya vizuri kwenye mzunguko wa pili ili wapate nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu.

Kifaru amesema kwamba pia uongozi wa klabu hiyo umepata mwaliko kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kwenda kucheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali ambazo wataandaliwa na wenyeji wao.

No comments