GEORGE LWANDAMINA APANGA KUCHUKUA UJUZI KWA HANS


Baada ya kutambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari kuwa ndie kocha mkuu wa Yanga hatimae George Lwandamina amesema kwamba amekuja katika klabu hiyo kwa nia ya kuifanya timu inapiga hatua katika maendeleo ya mpira wa miguu licha ya kuamini kuwa ana kazi kubwa ya kufanya ndani ya timu hiyo.

Lwandamina amesema kwamba anaamini atapata ushauri wa kutosha kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Hans van der Pluijm ili kwa pamoja kuendeleza pale walipoishia.

Amesema kwamba kwamba kwa sasa timu iko tayari na hakutakuwa na marekebisho makubwa kwani anaamini wachezaji waliopo bado wana nafasi ya kuisaidia timu kupiga hatua.
Hata hivyo Lwandamina amedai kuwa hakuna mazungumzo yeyote yanayohusiana na kusajili mchezaji kutoka klabu yake ya zamani ya Zesco kwa wakati huu hivyo hivyo atakuwa tayari kuzungumzia jambo hilo endapo kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo.

No comments