SIMBA WAKATAA KUCHEZA NA YANGA KATIKA MECHI ZIJAZO

Ungozi wa klabu ya Simba umesema kwamba kwa sasa hawatacheza mechi yeyote ile dhidi ya Yanga endapo TFF itaendelea kupanga waamuzi wa hapa nyumbani.

Mkuu wa mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema kwamba kama wao viongozi wameamua kufanya hivyo kwani waamuzi wa hapa nyumbani wamekuwa hawatendi haki kwa upande wao kwani mara nyingi hutoa maamuzi tofauti juu yao.

"Mfano mzuri ile mechi yetu dhidi ya Yanga,Martine Saanya anakataa goli halali la Ibrahimu Hajibu baadae anakubali goli la mkono lililofungwa na Amisi Tambwe,mwamuzi anatoa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa nahodha wetu Jonasi Mkude pasipo kosa lolote inashangaza sana"alisema Manara.

Amesema kwamba TFF kwa sasa inatakiwa kupanga waamuzi kutoka nje ya nchi katika mechi kubwa ya watani wa jadi ili kuondoa mzozo huo na wao watakuwa tayari kulipa gharama za waamuzi hao endapo TFF itashindwa kufanya hivyo.


No comments