LWANDAMINA AKABIDHIWA MAJUKUMU RASMI

Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Young Africans leo hii umemtambulisha rasmi George Lwandamina kuwa ndie kocha mkuu wa klabu hiyo akirithi mikoba ya Hans van der Pluijm aliyepewa jukumu la kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii katika makao makuu ya klabu mitaa ya Jangwani,makamu mwenyekiti wa Young Africans Clement Sanga amesema kwamba wamefikia maamuzi ya kuwatamburisha rasmi baada ya kwa pamoja kufikia makubaliano.
Amesema kwamba uongozi wa Yanga unamshukuru kocha Hans kwa hatua ambayo ameifikia wakati wa ufundishaji wake kwani ameifanya timu kuwa ni miongoni mwa vilabu bora kwa sasa hivyo wanaimani mrithi wake ataendelea kuendeleza pale alipoishia.

No comments