TIBOROHA AWAPONGEZA YANGA KWA KUMPA MAJUKUMU HANS

Katibu mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga Jonas Tiboroha ameupongeza uongozi wa klabu hiyo kwa hatua  ambayo wameifanya ya kumpa majukumu Hans kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Akiongea na MWANDIKE BLOGSPORT, Tiboroha amesema kwamba jambo hilo ambalo wamelifanya litaleta chachu ya maendeleo kwani mara nyingi virabu ambavyo vimefanikiwa huwa na wigo mpana katika benchi la ufundi.

"Viongozi wanastahili pongezi kwa hiki walichokifanya mpira wa sasa ni wa ushindani hivyo timu kuwepo na mkurugenzi wa ufundi ni muhimu na ukizingatia kocha Hans ni mzuri katika mambo haya ya mpira"alisema Tiboroha.

Amesema kwamba awali yeye akiwa katibu mkuu wa Yanga kulikuwepo na malengo ya kuwa na mkurugenzi wa ufundi lakini swala hilo halikuweza kutimia kutokana na sababu mbalimbali.

Katika hatua nyingine Tiboroha amewatoa hofu mashabiki wa Yanga kwa kusema kuwa nafasi ambayo amepewa kocha Hans kwani ana matumaini makubwa ya kuifanya kwa weledi kwani si mara ya kwanza yeye kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Amesema kwamba kinachotakiwa ni vyema viongozi wakampa ushirikiano wa kutosha na wamuache ayafanye majukumu yake pasipo shinikizo la aina yeyote juu ya yake.


No comments