YANGA WAIDAI TFFF ZAIDI YA MILIONI 200

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wa matawi ya Yanga,Bakili Makele umelitaka shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF kuwalipa fedha zao ambazo wanadai.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Bakili amesema kwamba TFF ilidiriki kukata fedha za Yanga baada ya mechi yao dhidi ya TP Mazembe ambazo wao kama wasimamizi wa soka hawakustahili kuzichukua fedha hizo.

Alisema kwamba TFF ilikata fedha zaidi ya milioni 200 kupitia VAT baada ya mashabiki kuingia bure kufuatia maagizo ya aliyekuwa mwenyekiti wa klabu Yusuf Manji akiwa madarakani, jambo ambalo halipo kisheria.

Aliongeza kwa kusema kuwa TFF inatambua hali iliyopo ndani ya klabu ya Yanga kwenye swala la uchumi lakini bado wanaendelea kuibana katika fedha ambazo walistahili kuzipata jambo ambalo linaonekana kuidhohofisha klabu hiyo.

Mbali na swala hilo,pia Bakili ameeleza kuhusiana na shirikisho hilo kushindwa kuwasimamia kupata vifaa vyao kwa wakati kutoka CAF baada ya kuingia hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ikiwa wao ndio wanaostahili kusimamia swala hilo.

Hata hivyo alisema kwamba kama TFF wanaidai Yanga basi wanapaswa kukata fedha hizo kwenye fungu lao la zaidi ya milioni 200 ambazo wanazidai lakini sio kuchukua pesa zao kupitia vyanzo vingine.



No comments