TFF WAIGEUKA YANGA MADAI YA ZAIDI YA MILIONI 200

Na Said Ally
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limeweka bayana juu ya kauli ya mwenyekiti wa matawi Yanga Bakili Makele aliedai kuwa klabu hiyo inaidai TFF zaidi ya shilingi milioni 200 hku pia wakishindwa kuwasadia katika kipindi hiki ambacho klabu haina fedha za kujiendesha.

Kaimu katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema kwamba madai ya mwenyekiti huyo wa matawi hayana msingi kwani kama wao wasimamizi wa soka hawawezi kukata pesa za klabu pasipo utaratibu sahihi.

Kidao alisema kwamba TFF ndio inaidai Yanga kiasi cha pesa zaidi ya shilingi milioni 100,000,000/ (milioni mia moja) ambazo waliwakopesha ili walipe baadhi ya mishahara wachezaji wao tangu mwezi wa 12 mwaka jana.

Alisema kwamba TFF pia iliwalipia tiketi za ndege kwenda Algeria baada ya kushindwa kupata fedha,huku akidai kuwa yapo mambo mengi wamekubaliana kuwasaidia Yanga ambapo TFF watakaikata klabu hiyo kupitia baadhi ya vyanzo vya mapato.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa yeye kama kaimu katibu mkuu wa TFF hawezi kuzungumza mambo mengi juu ya yale ambayo wameyafanya kwa klabu ya Yanga kwa sababu aliyetangaza kuwa Yanga inaidai TFF yuko nje ya mfumo rasmi wa klabu hiyo.

No comments