KABWILI AREJEA KIKOSINI NGORONGORO HEROES

Na Said Ally
Mlinda mlango wa timu ya Yanga,Ramadhani Kabwili ameungana na kikosi cha timu ya vijana ya Ngorongoro Heroes kinachojiandaa na mchezo wa kusaka kucheza fainali za Afrika dhidi ya Mali.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari Leo hii Rais wa Tff Wallace Karia alisema kwamba Kabwili amejumuika na wachezaji wenzake kambini kwa ajili ya kujiwinda na mchezo huo utakaopigwa siku ya jumapili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Alisema kwamba TFF ilifanya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Yanga kuhusiana na mchezaji huyo ambae awali aliondoshwa kikosini na kocha Ammy Ninje kwa madai ya kushindwa kuripoti kambini kwa wakati.

Aliongeza kwa kusema kwamba Kabwili kwa sasa yupo kambini na hakuna matatizo yeyote yaliyopo kati yake na kocha mkuu wa timu hiyo ya Taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes.

No comments