TFF YATOA ONYO KALI KWA MASHABIKI WATAKAOJIHUSISHA NA SIASA UWANJANI

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limetoa tahadhari kwa mashabiki wa mpira wa miguu hapa nchini ambao hapo kesho wanataraji kuingia uwanjani kushuhudia pambano la watani wa jadi Simba na Yanga kuachana na maswala ya siasa katika mchezo huo.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba,shirikisho hilo limepata taarifa zenye ukweli kuwa kuna baadhi ya mashabiki wana nia ya kuchana kadi ya chama kimoja cha siasa uwanjani sambamba na kuchoma bendelea ya chama.

Lucas amesema kwamba kwa yeyote mwenye dhumuni la kufanya hivyo ni vyema akasitisha jambo hilo kwani kwa yule atakaebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

No comments