SIMBA KUREJEA KESHO TAYARI KWA PAMBANO DHIDI YA YANGA

Kikosi cha timu ya soka ya Simba kinaendelea vyema na maandalizi ya kujiwinda na pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya watani zao Young Africans hapo siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mratibu wa Simba,Abasi Ally ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba wachezaji wote wako vizuri kwa hakuna mchezaji aliye majeruhi ambae huenda akakosekana kucheza kwenye pambano hilo.

Abasi alisema kuwa kikosi hicho kinataraji kurejea Dar es salaam siku ya kesho baada ya kukaa Zanzibar tangu wiki iliyopita wakijiandaa na pambano hilo la watani wa jadi.

No comments