MPIRA PESA WATAKA UMOJA KUWAFUNGA YANGA

Mwenyekiti wa Tawi la Simba la Mpira Pesa,Ostadhi Masoud amesema kwamba kwa upande wao kama wanachama wa wekundu wa Msimbazi wana chachu kubwa ya kupata ushindi kwenye pambano la watani wa jadi Simba na Yanga kwani ndilo litakalotoa mwanga wa atakaekuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu.

Masoud amesema kwamba umoja na mshikamano kwa wanachama wa klabu Simba ndio njia mojawapo itakayowafanya waibuke na ushindi hapo jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa mechi hiyo ya watani wa jadi huwa ina mambo mengi kuanzia nje ya uwanja hadi ndani ya uwanja hivyo umoja wao kwa wakati huo ndio utaleta tija ya ushindi kwenye pambano hilo linatarajiwa kupigwa siku ya jumamosi.


No comments