WANACHAMA WA YANGA WATAMBA KUIFUNGA SIMBA

Homa ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga ikiendelea kutawala katika kona mbalimbali hapa nchini,wanachama wa klabu hizo kongwe katika soka la bongo wamezidi kutambiana kwa kila mmoja akijinasibu timu yake kuibuka na ushindi kwenye pambano hilo la ligi kuu ya Tanzania bara litakalopigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Makamu mwenyekiti wa tawi la Yanga Tandale kwa Mtogele,Waziri Jitu ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kutokana na ubora wa kikosi cha timu hiyo na maandalizi yao kuelekea kwenye mchezo huo anaamini watafanikiwa kuibuka na ushindi wa kishindo.

Hata hivyo Jitu amewataka mashabiki wa Simba kuwa wastraabu kwenye pambano hilo na kuacha tabia ya kung’oa viti kwani uwanja huo ni mali ya Serikali na kila Mtanzania ana nafasi ya kuutumia.

No comments