MASHABIKI WA ZANZIBAR WAKOSA IMANI NA TIMU ZAO

Mashabiki mbalimbali wa visiwani Zanzibar kwa upande wao wamesema kwamba hawana matumaini makubwa ya timu moja wapo ya Zanzibar kuweza kufanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ya mapinduzi kwani viwango ambavyo wanavionyesha ni tofauti na timu za Tanzania bara.

Mashabiki hao wamesema kwamba timu hizo zinashindwa kufanya vizuri kutokana na kukosa wadhamini ambo wangeweza kutoa mchango mkubwa wa kuhudumia timu hizo kwa mahitaji mbalimbali.

Hata hivyo mbali na swala hilo pia wamekiomba chama cha soka Zanzibar ZFA kwenye michuano mingine kuweza kuongeza timu kutoka kisiwani Pemba na kuacha kasumba ya kuipa nafasi timu moja ya Jamhuri.

No comments