MAYANJA ARIDHISHWA NA MATOKEO YA SALE

Baada ya kulazimishwa sale ya bila kufungana dhidi ya timu ya URA ya nchini Uganda,kocha msaidizi wa timu ya soka ya Simba Jackson Mayanja amesema kwamba matokeo ambayo wameyapata ni mazuri kwao kwani wamefanikiwa kupata alama moja mbele ya timu ngumu.

Mayanja amesema kwamba vijana wake wameshindwa kuzitumia nafasi ambazo wamezipata lakini ana Imani watafanikiwa kufanya vizuri kwenye mechi zijazo na jambo la faraja kwao ni kuona bado wanaendelea kuongoza kundi lao.

No comments