AZAM FC WAMPONGEZA KIPA WA FRIKA LYON

Uongozi wa klabu bingwa Afrika Mashariki na kati,Azam Fc umesema kwamba umekubaliana na matokeo ambayo wameyapata katika mechi yao ya ligi kuu Tanzania bara mbele ya Afrika Lyon,ingawa matarajio yao ni kupata ushindi kwenye mechi hiyo iliyoisha kwa sale ya bila kufungana.

Msemaji wa timu ya Azam,Jafary Idd amesema kwamba kikosi chao hakikuwa na bahati ya kufanikiwa kupata ushindi kwenye mechi hiyo kwani wachezaji wa Azam kwa muda mrefu wamepanda kwa juhudi kubwa lakini mwisho wake wakashindwa kufanikiwa kupata goli.

Amesema kwamba matokeo ambayo wameyapata yametokana na ubora wa mlinda mlango wa Africa Lyon,kwani kwa kiasi kikubwa ameisadia vyema timu yake kuzuia mashambulizi yao.

No comments