IBRAHIM AJIBU RASMI YANGA

Uongozi wa klabu ya Yanga leo umemtamburisha rasmi mchezaji Ibrahim Ajibu baada ya kuingia kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara na michuano mingine.

Katibu mkuu wa Yanga,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba usajili huo ni matakwa ya kocha mkuu baada ya kubaini kiwango chake hasa alipokuwa katika timu ya Simba pamoja na timu ya Taifa.

Ajibu amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Matheo Anthony ambapo mchezaji huyo hatoonekana katika msimu ujao wa ligi kwenye klabu ya Yanga baada ya mkataba wake kumalizika.

No comments