AJIBU NA WENZAKE KUFANYIWA HAYA KABLA YA KUANZA MAZOEZI

Kikosi cha timu ya Yanga kinataraji kuanza rasmi maandalizi ya kujiwinda msimu ujao wa ligi siku ya jumatatu ya wiki ijayo.

Meneja wa timu ya Yanga,Hafidhi Salehe ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba kabla ya kuanza kwa mazoezi kocha mkuu wa timu hiyo amependekeza wachezaji wote waliosajiliwa hivi sasa na watakaobaki wapimwe afya zao, ambapo zoezi hilo limeshaanza kufanyiwa kazi.

Aidha katika hatua nyingine Hafidhi alisema kwamba kocha mkuu George Lwandamina amependekeza kikosi hicho kitoke nje ya mkoa wa Dar es salaam ili kupata wakati mzuri wa maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu.

Hata hivyo kwa mujibu wa daktari wa tiba za michezo Nassoro Ally Matuzya alisema kwamba hapo kesho wanataraji kuwapima afya wachezaji wa Yanga.

No comments