TASMA WATANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI

Kamati ya uchaguzi wa Chama cha wataalamu wa tiba za michezo (TASMA) imetangaza rasmi mchakato wa uchaguzi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika agost tano mwaka huu katika ukumbi wa manispaa ya Kinondoni.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari mwenyekiti wa uchaguzi Leslie Liunda alisema kwamba mwanachama yeyote anayopenda kukiongoza chama hicho anaombwa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea endapo kama atakuwa na sifa ambapo mchakato wa uchukuaji fomu unaanza rasmi hapo kesho.

Nafasi zinazogombewa ni nane.

Mwenyekiti
Makamu mwenyekiti
Katibu mkuu
Mweka hazina
Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF
Wajumbe wawili wa kamati ya utendaji.

No comments