OTIENO AWASIFU WACHEZAJI WAKE

Kocha wa timu ya Gor Mahia Zedekiah Otieno ameridhishwa na mafanikio ya kiwango cha wachezaji wake baada ya kufanikiwa kuwa mabingwa wa kwanza wa michuano ya SportPesa kwa kuwafunga wapinzani wao timu ya AFC Leopards kwa jumla ya mabao 3-0.

Otieno alisema kwamba mchezo wa leo ulikuwa na ushindani zaidi hivyo kufanikiwa kuwa mabingwa kwa upande wao ni jambo la kujipongeza.

Alisema kwamba kwa sasa wanarejea nchini Kenya kuendelea na majukumu mengine kabla ya kukabiliana na timu ya Everton endapo watapata nafasi ya kucheza nao.

No comments