TAIFA JANG'OMBE WAIVAA YANGA USAJILI WA NINJA

Uongozi wa timu ya Taifa Jang'ombe umeshangazwa na taarifa za klabu ya Yanga kumsajili mchezaji wao Abdallah Haji ikiwa mchezaji angali na mkataba na klabu hiyo wa muda mrefu.

Katibu wa timu hiyo Mohd Maulid alisema kwamba wao kama uongozi wamepata taarifa za kusajiliwa kwa mchezaji huyo baada ya kukamilisha mchakato mzima wa usajili kwa kupigiwa simu na viongozi wa Yanga.

"Tumepigiwa simu na uongozi wa Yanga wakituambia kuwa wanakuja siku ya jumamosi ili waje wamalizane na sisi,sasa tunashangaa endapo kama hatujaafikiana itakuaje wakati wao tayari wameshamsajili maana wao washafanya makosa"alisema Maulid.

Alisema kwamba kwa upande wao hawana kikwazo na mchezaji huyo kwani wanaamini kufanikiwa kwake kutasaidia kuimarisha timu ya Taifa ya Zanzibar ila kilichopo ni wao Yanga kufuata utaratibu wanaoutaka wao.

No comments