TFF WAMPONGEZA RAISI JOHN POMBE MAGUFULI

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limeipongeza Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuridhia kufunguliwa tena kwa uwanja wa Taifa ili utumike kwa ajili ya mechi za ligi kuu ya Tanzania bara.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari,Afisa habari wa shirikisho hilo,Alfred Lucas amesema kwamba kwa uamuzi huo ambao umefanywa na serikali chini ya Raisi John Pombe Magufuli kwao wameridhishwa mno na maamuzi hayo kwani itawapa fursa ya kuuendeleza vyema mpira wa miguu.

Hata hivyo Lucas amewataka mashabiki wa mpira wa miguu kuwa waungwana pindi waingiapo uwanjani hapo ikiwemo katika mechi ya kesho ya ligi itakayowakutanisha Simba na Azam.

No comments