RUVU SHOOTING BADO WAOTA KIPIGO CHA KILUVYA UNITED

Uongozi wa timu ya soka ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani,umesema kwamba kwa upande wao wamekubaliana na matokeo ya kufungwa na timu ya daraja la kwanza Kiluvya United,kwani ingawa hawakutegemea matokeo hayo lakini mpira ndivyo ulivyo mara nyingine huwa na maamuzi ya kikatili.

Afisa Habari wa timu hiyo,Masau Bwire amesema kwamba kwa sasa hawana cha kuzungumza Zaidi ya kushangazwa na matokeo ambayo yemewaondosha katika michuano ya kombe la FA.

"Hata mashabiki wa Kiluvya United walikuwa haamini kama wametufunga kwani wakati natoka uwanja nilikutana na kundi la mashabiki wa timu hiyo wakipeana taarifa za ushindi wao lakini chakushangaza wale waliopewa taarifa walijua wanadanganywa hadi hapo waliponipa simu kuwathibitisha kama ni kweli wametufunga nadhani hata wewe Said Ally umeshangazwa na matokeo haya."alisema Masau Bwire.

Amesema kwamba kwa sasa kikosi kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara ambapo leo hii wameanza safari ya kuelekea Mwanza kwa ajili ya mechi hizo.

No comments