SIMBA WAELEKEZA NGUVU ZAO KWA AZAM FC

Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-0 mbele ya timu ya Polisi Dar es salaam katika michuano ya kombe la FA,uongozi wa Simba umesema kwamba kwa sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Azam FC.

Meneja wa Simba Mussa Hassani Mgosi amesema kwamba kwa sasa kikosi kinaendelea vyema na maandalizi kwa ajili ya mchezo huo kwani dhamira yao ni kuona wanapata alama tatu kwa ajili ya kuendelea kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo ili kutimiza azma yao ya kuwa mabingwa.

Amesema kwamba wachezaji wote wapo katika hali nzuri na habari njema ni kulejea kwa kiuongo wao mahili Mohamed Ibrahim anayetarajiwa kuanza mazoezi hapo kesho.

"Kikubwa mashabiki waendelee kuwa na mshikamano wa pamoja kwani kufanya hivyo kutaifanya Simba itimize azima yake ya kuchukua makombe yote mawili la ligi pamoja na FA"alisema Mgosi.

No comments