POLISI DAR ES SALAAM WATINGA TFF KUIONDOSHA SIMBA

Uongozi wa timu ya soka ya Polisi Dar es salaam inayoshiriki ligi daraja la kwanza umeendelea kutoa ufafanuzi juu ya rufaa yao waliyokata TFF kuhusiana na klabu ya Simba kumchezesha mchezaji Novat Lufunga kwenye mchezo wa kombe la FA ili hali hakustahili kucheza kwenye mechi hiyo kwa kuwa ana adhabu ya kutumikia kadi nyekundu aliyeipata msimu uliopita kwenye mchezo wao dhidi ya Coastal Union.


Insepekta Jodarn ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba ni kweli uongozi wa klabu hiyo umewasilisha rufaa hiyo ikipinga kitendo cha Simba kumchezesha mchezaji mwenye adhabu ya kutumikia kadi,hivyo kwa sasa wanaendelea kusubiri maamuzi ya TFF juu ya swala hilo.

"Sisi tumejiridhisha kuwa Lufunga hakustahili kucheza kwenye mechi yetu maana unakumbuka ndugu mwandishi kuwa mchezaji huyo alipewa kadi kwenye mechi dhidi ya Coastal Union ya msimu uliopita na kanuni inazuia kufanya hivyo" alisema Jodarn.

No comments