MWAMUZI ALIYECHEZESHA MECHI YA MAJIMAJI NA YANGA AONDOLEWA

TFF imemuondoa mwamuzi Hussein Athumani, kwenye orodha ya waamuzi wa ligi kuu ya Tanzania bara, baada ya kupata alama za chini ambazo haziwezi kumuezesha kuendelea kuchezesha michezo ya ligi hiyo.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari,Afisa habari wa TFF,Alfred Lucas amesema mwamuzi huyo aliyechezesha pambano kati ya Majimaji na Yanga katika mechi iliyochezwa Songea ameshindwa kutafasiri vyema sheria 17 za mpira wa miguu hapa nchini.

Amesema kwamba mbali na mwamuzi huyo,pia timu ya Yanga imepigwa faini ya shilingi milioni moja kwa kitendo cha timu hiyo kutoingia vyumbani na pia kutumia mlango ambao sio rasmi wakati wa kuingia uwanjani.


No comments