AFRIKA LYON WAJINASIBU KUWAFUNGA YANGA

Uongozi wa timu ya soka ya Afrika Lyon ya jijini Dar es salaam,umesema kwamba kikosi chao kinaendelea vyema kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kuchezwa siku ya ijumaa kwenye uwanja wa Uhuru dhidi ya Young Africans.

Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo Charles Otieno amesema kwamba kwa upande wao msimu huu wamejipanga kufanya vizuri kwa mechi zote,kwani nia yao ni kupata pointi tatu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi.

Otieno amesema kwamba wanafahamu kuwa Yanga ni wazuri,lakini hilo haliwapi hofu yeyote kwani kikosi chao kimejiandaa kikamilifu kuhakikisha kuwa wanapata alama tatu muhimu.

No comments