KWIHAVA APANGA KUIPELEKA LIGI KUU LIPULI

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa,Spiani Kwihava,amesema kwamba baada ya kufanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti katika chama hicho, kwa sasa mipango yake ni kutimiza ahadi zake ikiwemo kupata viwanja bora kwa kila wilaya na kukuza soka la vijana na wanawake mkoani humo.

Kwihava amesema kwamba dhumuni lao kubwa ni kutimiza vipao mbele vitatu ambavyo walivieleza hapo awali,kwani nia yao ni kuona mkoa huo unakua na chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

Aidha amesema kwamba mbali na maswala hayo pia mipango yao ni kuona timu ya Lipuli ya mkoani humo ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza,msimu ujao ipate nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments