TFF YATOA ONYO KALI KWA WACHEZAJI WASIO NA VIBALI

Baada ya idara ya Uhamiaji kuwataka viongozi wa vilabu vya Simba,Yanga na Azam kuwakamilishia wachezaji na makocha wa kigeni kupata vibali vya kufanya kazi hapa nchini ili kukidhi matakwa ya katiba ya nchi,leo hii shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba katika mechi zijazo za ligi kuu ya Tanzania bara mchezaji asiye na kibali hataruhusiwa kucheza mechi hizo.

Katibu mkuu wa TFF,Selestine Mwesigwa amesema kwamba kama wao wasimamizi wa mpira wa miguu hapa nchini wamekuwa wakilisimamia swala hilo kwa weledi mkubwa hivyo wanashangaa viongozi wa vilabu ambavyo wameshindwa kufanikisha swala hilo.

Mwesigwa amesema kwamba ametoa agizo kwa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuhakikisha kuwa anawapa taarifa makamisaa wa michezo yeto inayofuata kukagua mahitaji yanayohitajika kwa wachezaji wa kigeni.

Hata hivyo idara ya uhamiaji imewataka viongozi wa vilabu ambavyo wachezaji wao hawana vibali vinavyowafanya kuishi hapa nyumbani kushugulikia swala hilo mara moja kwani,wasipofanya hivyo watachukuliwa hatua kali ikiwemo kuwakamata na kuwapeleka mahakamani.

No comments