IDYOSA WAPATA MWALIKO WA KUCHEZA NA TIMU ZA KENYA

Uongozi wa chama cha Soka cha vijana wilaya ya Ilala Idyosa umesema kwamba umepata mwaliko kwa timu zao za wilaya hiyo kucheza michezo ya vijana na baadhi ya timu kutoka nchini Kenya baada ya mkurugenzi wa kituo cha Spaya Mambo Sasa kufanikisha shughuli hiyo.

Mwenyekiti wa Idyosa Father Edwini Mloka amesema kwamba timu nne za vijana kutoka nchini Kenya zinataraji kucheza michezo mbalimba na timu za vijana wa Idyosa kwa lengo la kuleta tija kwenye maendeleo ya mpira wa miguu.

Amesema kwamba michezo hiyo inataraji kuanza leo hii kwenye kituo cha kukuza vipaji cha Jakaya Kikweto huku pia wakitaraji kutumia viwanja mbalimbali kwa ajili ya michezo hiyo itakayodumu kwa siku tatu.

No comments