TAIFA STARS BADO HAIJAANZA MAZOEZI RASMI

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba asilimia kubwa ya wachezaji ambao wameitwa kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe wameshalipoti kambini.

Mkwasa amesema kwamba kwa sasa wachezaji ambao hawajalipoti kambini ni wachezaji wa timu ya Yanga na Ruvu Shooting ambao watajiunga mara baada ya kumaliza majukumu yao katika timu zao.

Amesema kwamba licha ya kuwasili kwa wachezaji hao lakini hawajaanza mazoezi kwani idadi kubwa walichelewa kufika kambini na baadhi yao wanashughulikia maswala ya pasipoti.

Hata hivyo amesema kwamba kwa ujumla maandalizi sio mazuri sana kwa kuwa kikosi hakijapata muda wa kufanya mazoezi hii inatokana na wachezaji walioitwa kuwa katika majukumu kwenye timu zao.

No comments