NAPE AWATAKA WADAU WA MICHEZO KUTOKWENDA MAHAKAMANI

Waziri mwenye dhamana ya Michezo hapa nchini,Nape Nnauye amewataka wadau wa michezo kuacha tabia ya kwenda Mahakamani,kwani kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira.

Amesema kwamba kumekuwa na migogoro mingi hasa katika chaguzi mbalimbali za viongozi wa vyama husika na matokeo yake hujikita kupelekana mahakamani pasipo kutambua taratibu husika.

 Nape ameyasema hayo kufuatia taarifa za baadhi ya wadau wa mchezo wa riadha kutaka kwenda mahakamani kwa madai kuwa uchaguzi wa chama hicho haukufuta katiba.

No comments