SAMATA KUWASILI SAA SITA USIKU

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samata anatarajiwa kuwasili saa sita usiku wa leo kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu hiyo katika harakati za kujiwinda na mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mara baada ya kutua kwa mchezaji huyo moja kwa moja atajiunga na wachezaji wenzake ambao baadhi yao tayari washaripoti kambini.

Lucas amedai kuwa kwa asilimia kubwa maandalizi ya timu hiyo yamekamilika na kwa sasa wanasubiriwa wachezaji ambao siku ya kesho watavitumikia vilabu vyao katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments