ZARI AACHANA RASMI NA DIAMOND
Na Mwandishi wetu,
RASMI MAPENZI SASA BASI! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Zari a.k.a the Lady Boss kutangaza rasmi kutemana na mzazi mwenzake Diamond Platnumz.
Siku za hivi karibuni kulizuka taarifa za kuwa penzi la wawili hao limeingia kidudu na linaelekea kufika mwisho na hii ni baada ya mkasa wa Dimond kukubali kuzaa na msanii wa Bongo Movie, Hamisa Mobeto.
Zari ameamua kuwatangazia mashabiki wake kuwa yeye ndie aliamua kuachana na Dimond kutokana na kukerwa na tabia zake za usaliti wa kimapenzi.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Mwandike.blogspot,imebaini ujumbe aliouandika Zari ambao ulieleza sababu zote hizo zilizomfanya kufikia maamuzi hayo licha ya kuwa yeye na Diamond wamezaa watoto wawili Nillan na Tiffah.
“Elewa kuwa hiki ni kitu kigumu sana kwangu kukifanya, kumekuwa na tetesi mbalimbali baadhi kati ya hizo zimekuwa na ushaidi ambao umekuwa ukisambaa katika vyombo vya habari kuhusiana na usaliti wa kimapenzi unaofanywa na Diamond, kwa huzuni nimeamua kuvunja uhusiano wangu wa kimapenzi na Diamond kwa heshima yangu”
“Tunaachana kama wapenzi lakini sio kama wazazi hii hainipunguzii mimi kuwa mtu wa kujitegemea, mama mwenye kujali na Boss Lady, wote mnatakiwa kufahamu hilo nitaendelea kujijenga kama mwanamke mwenye ushawishi, nitawaamasisha wanawake wote kuwa maboss Ladies”
“Nitawafundisha watoto wangu wanne wa kiume kuwaheshimu wanawake na nitamfundisha binti yangu ni nini maana ya heshima, nimekuwa katika kiwanda cha burudani kwa miaka 12 sasa pamoja na changamoto zote hizo lakini nimefanikiwa kuwa mshindi kwa sababu mimi ni mshindi nawatakiwa wote siku njema ya wapendanao”

Post a Comment