YANGA KUWAFUATA ST LOUIS KWA TAHADHARI KUBWA

Na Said Ally
Kikosi cha timu ya Yanga kinataraji kuelekea nchini Shelisheli siku ya jumapili kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa kombe la klabu bingwa barani Afrika dhidi ya  St Louis.

Msemaji wa timu ya Yanga,Dismas Ten amesema kwamba kikosi kinaenda katika visiwa hivyo vya Shelisheli kwa tahadhari kubwa kwani nia yao ni kupata matokeo mazuri ambayo yatawapa nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Dismas alisema kwamba wapinzani wao St Louis si timu ya kubeza kama ilivyokuwa inaelezwa hapo awali kwani kila mdau wa mpira anaamini amegundua ubora wao.

Aidha katika hatua nyingine Dismas alisema kwamba kikosi hicho pia kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Majimaji.

Alisema kwamba mchezo huo utapigwa siku ya jumatano jijini Dar es salaam na wao wamejipanga kikamilifu kuchomoza na ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments