YANGA KWENDA SHELISHELI BILA YA CHIRWA

KIKOSI cha Yanga Sc  kinatarajia kusafiri kesho asubuhi kueleka Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano na wenyeji  St Louis Fc kwenye ligi ya mabingwa afrika mchezo ulipangwa  kuchezwa jumatano ijayo Stade Liete.

Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten ameiambia Saidaallymwandike.blogsport.com kuwa  jumla ya nyota 20 na viongozi 10 kati yao 8 kutoka benchi la ufundi watasafiri asubuhi ya kesho  kupitia Nairobi tayari kwa mchezo huo muhimu  siku ya jumatano.

Ten alisema kuwa, wachezaji  Thabani Kamusoko ambaye amepona majeraha yake hivi karibuni na kuanza mazoezi mepesi pia ameondolewa kutoka orodha ya nyota ambao wangesafiri kueleka Shelisheli ili apate muda wa kujifua zaidi na kurejesha makali yake, sambamba na  Obrey Chirwa ambaye naye  hayumo kwenye orodha ya wachezaji watakaosafiri kwa sababu ya maumivu ya misuli aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Majiamaji.

Orodha ya wachezaji ambao watasafiri hapo kesho kwenda Shelisheli.

Ramadhani Kabwili,Beno Kakolanya,Youthe Rostand,Hassan Kessy,Juma Abdul,Mwinyi Haji,Gadiel Michael,Nadir Haroub,Patto Ngonyani,Kelvin Yondani,Said Juma,Papy Tshishimbi,Pius Buswita,Raphael Daud,Yussuf Mhilu,Ibrahim Ajib,Said Mussa,Emmanuel Martin,Geoffrey Mwashiuya,Juma Mahadhi.

No comments