SIMBA WAMTAMBURISHA RASMI KOCHA WAO MWENYE REKODI YA KUIPA CAMEROON MEDALI YA DHAHABU

Na,John Luhende
Klabu ya Soka ya Simba leo imemtambulisha rasmi kocha wao mpya Mfaransa Pierre Lechantre, Kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Habib ambao wanaenda kuungana na Kocha Msaidizi, Mrundi Masoud Djuma kukinoa kikosi hicho ambacho kinaongoza msimamo wa Ligi Kuu bara wakiwa na pointi 29.

Kocha huyo ametambulishwa mbele ya wandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo Meneja wake aliefahamika kwa jina la Joseph ambaye alielezea namna ambavyo Simba ilifanikiwa kumnasa kocha huyo ambaye moja ya mafanikio yake katika soka la Afrika ilikuwa ni ubingwa wa Mataifa ya Afrika aliyotwaa akiwa kama Kocha wa Timu ya Taifa ya Cameroon mwaka 2000.

Lakini pia sifa nyingine ya Lechantre ni kuiongoza Timu ya Taifa ya Cameroon kushinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki nchini Ugiriki mwaka 2001 akiwa kama Mkurugenzi wa Ufundi.

Uteuzi wa Mfaransa Lechantre umefanyika baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Mcameroon Joseph Omog ambaye licha ya kuiongoza Simba katika michezo ya awali ya mzunguko wa kwanza akiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi alifungashiwa virago vyake na nafasi yake kukaimu Kocha msaidizi raia wa Burundi, Masoud Djuma.

Katika tukio hilo la kutambulishwa Kocha Lechantre alisaini mkataba wa kuifundisha Klabu hiyo kongwe lakini ukiwa na makubaliano ya kutowekwa wazi mbele ya wandishi wa habari.

Mfaransa huyo ataanza kukinoa kikosi cha Simba baada ya Timu hiyo kurejea jijini Dar es Salaam ikitokea mkoani Kagera ambapo itacheza na Kagera Suger jumatatu ya wiki ijao katika uwanja wa Kaitaba.
nilishuhudia Timu ikicheza na kupata ushindi, ni jambo zuri na nilifarijika kuiona Timu ikiwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini uwepo wangu hapa naamini utaiongezea kitu kikubwa Klabu.

"Ni vema mkasahau wasifu wangu na kuniacha nifanye kazi ili niweze kuisaidia Timu yetu kufanya vema haswa katika michuano ya Kimataifa, naamini kwa kushirikiana na Kocha Msaidizi, Djuma tutaweza kuifanya Simba iliyo bora na yenye uwezo wa kupambana kimataifa," alisema Kocha Lechantre.

No comments