BENO KAKOLANYA AMALIZANA NA YANGA

Na,Said Ally
Mlinda mlango wa timu ya Yanga,Beno Kakolanya amesema kwamba kwa sasa tayari amesharejea katika kikosi cha timu hiyo baada ya uongozi kumlipa stahiki zake ambazo alikuwa anazidai katika klabu hiyo.

Kakolanya ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT,kwamba uongozi umekamilisha kila kitu ambacho alikuwa anakidai hivyo kwa sasa amerejea kikosini na tayari ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake tangu waliporejea kutoka Zanzibar.

Awali Kakolanya aliweka shinikizo la kutokuwepo katika kikosi cha Yanga hadi hapo atakapokamilishiwa fedha zake usajili ambazo alikuwa bado hajamaliziwa na uongozi wa klabu hiyo.

No comments