MWAKYEMBE AWAAMBIA HAYA SIMBA KUHUSU MABADILIKO

Na,Said Ally
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe ameutaka uongozi wa klabu ya Simba kukaa na mwekezaji wa klabu hiyo ili kumuelewesha namna ya matakwa ya serikali juu ya umiliki wa Hisa kwa vilabu vya wanachama.

Mwakyembe alisema kwamba kanuni za serikali ambazo zimetolewa kwa vyama vya soka na mashirikisho zinaeleza kuwa klabu za mpira wa miguu ambazo zimeanzishwa na wanachama mwekezaji anapaswa kumiliki Hisa za asilimia 49 huku wanachama watakuwa na asilimia 51.

"Sio swala la sisi kukubaliana, sisi ni Serikali tunasubiri hiyo 49 ndiyo tunayoitambua kwa hiyo ni swala la Simba wenyewe kukaa ndani kukaa na mwekezaji kumuelewesha haki zake nafasi yake ambayo sisi tunajua ni kubwa tu,wakitaka msada wetu sisi tuko tayari kumuelewesha muwekeza kwamba bado ana nafasi ile na tunathamini mchango wake"alisema Mwakyembe.

Aidha alisema kwamba kwa upande wao kama serikali hawatafanya mabadiliko yoyote juu ya umiliki wa Hisa hizo kwa vilabu vya wanachama kwa kuwa tayari zilishapitishwa tangu mwaka jana na vyama husika vishapatiwa kanuni hizo hivyo ni vyema vilabu husika vinavyotaka mabadiliko kufuata kanuni zilizowekwa na serikali.

Mwakyembe aliyasema hayo baada ya leo hii kukutana na kaimu raisi  wa klabu ya Simba Salim Abdalah katika kikao cha pamoja kujadili swala mabadiliko ya uendeshaji wa timu kwenda katika mfumo wa Hisa hii imetokana na awali uongozi wa klabu hiyo kuhitaji kufanya mazungumzo na waziri juu ya jambo hilo.

No comments